Kikosi cha Manchester United kimeibuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Leeds ya Australia ambapo mashetani hao wekundu wameweka kambi nchini humo kwaajili ya msimu ujao.

Kwa upande wake mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford  ameibuka mchezaji bora wa mchezo dhidi ya timu hiyo kwenye mtanange huo ambapo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Kocha mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa ameshangazwa na uwezo wa Rashford ambaye amefunga bao pamoja na kinda Mason Greenwood ambaye ametupia bao lake la kwanza, mabao mengine yalifungwa na Phil Jones pamoja na Martial.

Mchezaji aliyechaguliwa na mashabiki kuwa mchezaji bora kwa mchezo ni kiungo mshambuliaji Paul Pogba raia wa Ufaransa kwa uwezo ambao aliuonesha katika mchezo huo na kuisaidia timu yake kupata ushindi huo mnono.

Manchester United wanakabiliwa na changamoto ya kuimarisha upya kikosi chao ambacho kilimaliza msimu uliopita bila ya kunyakua taji lolote pia wakikosa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu ujao.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 18, 2019
Hamilton abakiza hatua chache kumfikia Michael Schumacher