Mshambuliaji Marcus Rashford ameongeza matumaini ya Manchester United kumaliza katika nafasi ya nne bora kwenye Ligi Kuu England kwa kurejea mazoezini.

Mshambuliaji huyo wa England, Rashford, ambaye amefunga mabao 29 msimu huu, alikosa kwenye ushindi wa mabao 2-0 katika mechi iliyopita dhidi ya Wolves kutokana na jeraha la mguu.

“Kuna habari njema kuhusu Marcus Rashford na Scott McTominay, ambao wote wamerejea mazoezini,” taarifa ya United ilisomeka baada ya kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag kufanya mazoezi Carrington hapo juzi.

“Mfungaji wetu anayeongoza alishiriki kwenye mazoezi baada ya kukosa ushindi dhidi ya Wolves kutokana na jeraha.”

Kiungo wa kati wa Scotland McTominay pia anakaribia kurejea, akiwa hajacheza tangu tangu Aprili 8, mwaka huu alipofunga bao katika ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Everton.

Beki wa Ufaransa Raphael Varane, ambaye Ten Hag alisema alibadilishwa baada ya kuchelewa dhidi ya Wolves kama tahadhari, pia alifanya mazoezi Jumatano.

Baada ya safari yao katika pwani ya kusini, United inahitimisha kampeni yao ya ligi kwa mechi za nyumbani dhidi ya Chelsea na Fulham.

Mashabiki Simba SC waombwa utulivu
Polisi Tanzania yaitumia salamu Simba SC