Mwanaume mmoja nchini Msumbiji, Irmao do Jovem amelazimika kulipa mahari ya mke wake aliyefariki kutokana na matatizo ya kujifungua.

Kijana huyo amelazimika kulipa mahali baada ya ndugu wa marehemu mke wake kumlazimisha kulipa ”Lobolo” kwa kutishia kwamba la sivyo hatozikwa.

Hali hiyo imetokana na kijana huyo kushindwa majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea, hivyo ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefarik.

Pia kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya haruasi, ambapo familia ya kijana huyo imekubali kulipa lakini pia imeshutumu tabia ya marehemu huyo, ameeleza ndugu wa kijana huyo Irmao do Jovem.

”Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi”.

Mbaraka Yusuph Aipa Mtihani Mzito Azam FC
74 Wachukua Fomu, Kurejesha TFF