Baada ya kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.

Marekani imetoa msimamo huo dhidi ya Uingereza kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry amesema hayo katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond

Pamoja na hayo Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.

John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.

Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla

Iceland Wamlazimisha Roy Hodgson Kujiuzulu
Kocha Wa TP Mazembe Awajibu Young Africans