Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Democratic leo limepitisha muswada wa sheria wa kufanya mageuzi mapana ya shughuli za polisi kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika hivi karibuni kushinikiza mabadiliko kwenye idara za polisi nchini humo.

 Muswada huo sasa utapelekwa mbele ya Baraza la Seneti ambako chama cha Republian kilicho na wajumbe wengi kimesema kitapinga mageuzi hayo yanayolenga kupunguza ukatili wa polisi, kuongeza mafunzo pamoja na kuimarisha uwajibikaji katika ngazi ya kitaifa.

Muswada huo pia unapiga marufuku mbinu ya polisi kuwakaba kooni wahalifu , kukomesha ukamataji wa watu bila kibali, kuongeza matumizi ya kamera za kunasa matukio na kuanzisha rikodi ya taifa ya kufuatilia matendo ya maafisa wa polisi.

Ikumbukwe kuwa Maandamano dhidi ya ukatili wa polsii na mfumo unaokumbatia ubaguzi nchini Marekani yalichochewa na kifo cha mmarekani mweusi George Floyd kilichotokea mwezi Mei baada ya kukandamizwa shingoni na polisi mmoja mzungu.

NEC yafunguka tarehe ya uchaguzi mkuu
JPM Arejesha Meli Bukoba, majaribio juni 28