Rais wa Marekani Donald Trump amemshinikiza gavana wa Republican wa jimbo la Georgia kumsaidia kupindua ushindi wa Joe Biden jimboni humo.

Katika mfululizo wa ujumbe aliotuma kupitia mtandao wa Twitter, Donald Trump amemtaka mgombea Brian Kemp kuitisha kikao maalum cha bunge.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Trump kuhudhuria mkutano wa kampeni huko Georgia wakati jimbo hilo linajitayarisha katika marudio ya uchaguzi wa seneti.

Trump, bado hajakubali kushindwa katika uchaguzi mkuu akidai kulikuwa na wizi wa kura ingawa hajawahi kutoa ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ushindi wa Biden ulitokana na wizi wa kura.

Hata hivyo Trump amefungua kesi mahakamani katika majimbo kadhaa nchini humo lakini hadi kufikia sasa kesi zote zimeshindwa kufaulu.

Jimbo la Georgia lilikuwa ngome muhimu katika uchaguzi huo ambapo Joe Biden aliibuka na ushindi mdogo ikiwa ni mara ya kwanza jimbo hilo linampigia kura mgombea urais wa chama cha Democrat tangu mwaka 1992.

EU na Uingereza ngoma bado nzito
Nditiye: Wazazi walindeni watoto kipindi cha likizo