Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa nchi yake inapanga kutoa majibu kuhusiana na shambulio la kemikali lililotokea katika mji wa Douma nchini Syria.

Ameyasema hayo mara baada ya kutolewa kwa kauli mbalimbali za kulaani shambulio hilo zilizotolewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Marekani katika baraza hilo, Nikki Haley amemtuhumu Rais wa Syria, Bashar al Assad kwa jinsi alivyowajibika kwa shambulio hilo.

Aidha, Mwakilishi wa Urusi, Vassily Nebenzia amesema tukio lililotokea katika mji wa Douma ni la kupangwa, na kwamba hatua za kijeshi zinazotaka kuchukuliwa na Marekani zinaweza kuwa na athari mbaya zaidi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar Jafari amesema kuwa Marekani na washirika wake wamekuwa wakifadhili ugaidi nchini Syria, na ndio wao wanaopaswa kuwajibika na shambulio hilo la kemikali.

Hata hivyo, kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kauli iliyotolewa na Rais, Donald Trump, kumekuwa na dalili zinazoonyesha kuwa mataifa ya magharibi yataungana na Marekani kupanga hatua za kuchukua.

Kesi ya kuondolewa ukomo wa umri wa urais Uganda 'yawaka'
Video: CCM waparurana bungeni, Ndugai aeleza kunusa kifo India