Marekani imekubali kusambaza misaada ya kijeshi nchini Israel ndani ya miaka 10 ijayo kwa mkataba wa dola bilioni 38, mkataba huo ni mkubwa katika historia ya Marekani.

Katika mkataba huo Israel watapokea dola milioni 500 kwa mwaka kwa ajili ya mpango wa ulinzi wa makombora.

Israel wanatakiwa kufanya makubaliano kadhaa na Marekani ya kupata fedha ikiwemo makubaliano ya kutochukua fedha za ziada kutoka Congress na kuahidi kuwa hawatatumia fedha za msaada kwa ajili ya ulinzi wake mwenyewe

Makubaliano hayo yamekuja baada ya miezi kumi ya mazungumzo kati ya Israel na Marekani.

Rais Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanaweza kukutana kwa mazungumzo katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini New York

Wabunge wakatwa Posho ya Siku ‘kuwashika mkono’ wahanga wa tetemeko la Ardhi
Ligi Ya Mabingwa Ulaya UEFA Yaanza Kutimua Vumbi