Marekani imesema kuwa inapanga kupiga marufuku raia wake kusafiri kuelekea Korea Kaskazini, kwa mujibu wa mashirika mawili ya kupanga safari ambayo yanafanya kazi nchini humo.

Mashirika hayo yanayojihusisha na safari nchini humo ni Koryo Tours na Young Pioneer Tours ambayo yamesema kuwa amri hiyo ya kupiga marufuku safari za kuelekea Korea Kaskazini itatangazwa tarehe 27 Julai mwaka huu na kuanza kutekelezwa siku 30 baadaye.

Aidha, Kampuni ya Young Pioneer Tours ndio iliyofanikisha safari ya mwanafunzi Mmarekani, Otto Warmbier kwenda Korea Kaskazini kwaajili ya masomo kabla kukamatwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka 15 na baadaye kurejeshwa Marekani akiwa amepoteza fahamu kabla ya muda mfupi kuaga dunia.

Hata hivyo, Kampuni hiyo yenye makao makuu yake nchini China imesema kuwa haitajihusisha tena kutoa msaada kwa Wamerekani kuingia Korea Kaskazini ili kuweza kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

Kampuni hiyo imetoa taarifa hiyo na kusema kuwa wamepewa taarifa kuwa Serikali ya Marekani imepanga kupiga marufuku raia wake kwenda nchini Korea Kaskazini, ingawa Marekani bado haijasema chochote kuhusu jambo hilo.

Lissu achukuliwa vipimo vya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali
LIVE: Rais Magufuli akizindua ujenzi wa barabara Kasulu, Kigoma