Mshirika wa Rais Donald Trump, pia ni afisa wa ngazi ya juu wa chama cha Republican, ambaye ndiye kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti La Marekani Mitch McConnell, amempongeza Joe Biden kwa ushindi wake katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Senata McConnell, alizungumza baada ya wajumbe wa uchaguzi ‘electoral college’ kuidhinisha rasmi ushindi wa Biden dhidi ya Rais Trump.

Trump, bado amekataa kukubali kushindwa huku akiendelea kutoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura katika kipindi cha uchaguzi.

”Mahusiano ya na bunge la Seneti ambalo kwa sasa linadhibitiwa na republican, yatakuwa muhimu kwa urais wa Biden”.

Rais wa Marekani hachaguliwi mara moja na wapigakura, bali kwa kile kinachoitwa electoral college.

Simiyu: Tarura yadai halmashauri Sh mil 130
Kocha Kaze akabidhi jalada kamati ya usajili Young Africans