Hatimaye Marekani imeingia kwenye historia nyingine ya masuala ya utabibu baada ya Hospitali ya Mjini Boston kuwa ya kwanza nchini humo kufanikiwa kufanya operesheni ya kupandikiza uume.

Jopo la Madaktari wa hospitali hiyo wamefanikiwa kumpa furaha tena Thomas Manning mwenye umri wa miaka 64 aliyepewa kiungo hicho muhimu, baada ya kugundulika kuwa uume wake ulikuwa umeathiriwa na saratani.

Manning amekuwa mtu wa tatu duniani kufanyiwa upasuaji huo na kufanikiwa kwa kiwango kilichotarajiwa.

Dk. Dicken Ko, ambaye ni mmoja kati ya madaktari waliofanikisha zoezi hilo aliiambia BBC kuw wanaume wengi wamekuwa wakipata athari za kisaikolojia zinazoathiri maeneo nyeti lakini wengi hawapendi kufahamika.

Video: Museveni adaiwa kumuandaa mwanae, ampaisha jeshini
Mjane aliyemlilia Rais Magufuli akabidhiwa nyumba, Shamba

Comments

comments