Marekani imesema kuwa inawashughulikia wahalifu wote wa mitandaoni ambao wamesababisha usumbufu mkubwa dhidi ya watumiaji wa mitandao hiyo.

Nchi hiyo imefikia hatua hiyo mara baada ya wahalifu hao kuingilia mfumo wa Kompyuta duniani na kuwataka watumiaji kulipa kiasi cha dola mia tatu ili waweze kurejeshewa huduma zao.

Aidha, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani imewataka watumiaji wa Kompyuta duniani kote kutolipa kiasi hicho cha fedha kwani inauwezo wa kupambana nao.

Hata hivyo, nchi hiyo imeongeza kuwa uhalifu wa kimtandao umeanzia katika nchi ya Ukrine na kusambaa duniani kote ambapo mashirika mbali mbali na taasisi za kifedha zimeathirika kwa kiasi kikubwa.

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 28, 2017
Video: Ni ulinzi wa 'kufa mtu' mahojiano ya Lowassa, Umeme wa uhakika wanukia