Rais wa Iran, Hassan Rouhani amepinga vikali kauli ya Marekani iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo aliyesema kuwa taifa lake linatarajia kuiwekea Irani vikwazo ambavyo havijawahi kuvipitia katika historia ya taifa hilo.

Rouhani amesema Pompeo, alipokuwa mkuu wa shirika la upelelezi la CIA, alishawahi shinikiza kuwekwa vikwazo dhidi ya taifa hilo ili kuachana na silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.

“Wewe ni nani uweze kuwa na maamuzi dhidi ya Iran ambayo ni nchi yenye uhuru wake na dunia kwa ujumla,”amesema rais wa Iran

Kwa upande wake waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu amepongeza kauli ya waziri wa mambo ya nje Pompeo na uungwaji mkono wa Marekani.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo ametaja mambo kumi na mbili ambayo Washington inautaka utawala wa Tehran kufanya, ikiwa ni pamoja na suala la Iran kuondoa vikosi vyake, Syria na kusitisha misaada kwa waasi wa Yemen.

 

 

 

Video: Vigogo CCM matumbo joto, Sugu asimamisha mkutano Bunge
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 22, 2018