Marekani imeionya Saudi Arabia dhidi ya shambulio la angani lililolenga sherehe za  mazishi nchini Yemen na kuwaua zaidi ya watu 140 na wengine wengi kujeruhiwa.

Imesema kuwa, mashambulio ya angani, yalioongozwa na majeshi ya muungano chini ya Saudi Arabia  katika mazishi hayo.

Mfanyakazi  wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Yemen,  Jamie McGold-rick, amesema kuwa wafanyikazi wa utoaji misaada, wameshtushwa sana na shambulio hilo, lililofanyika katika mji mkuu Sanaa.

Waombolezaji walikuwa wakitoa heshima zao za mwisho, kufuatia kifo cha babake kinara  maarufu wa waasi.

Marekani imesema kuwa, inatathmini kupunguza uungaji wake mkono wa majeshi hayo ya muungano yanayoongozwa na Saudi Arabia.

Saudi Arabia, imekanusha kuwa ndege zake zilishambulia mkutano huo wa mazishi.

#MdahaloUrais: Trump asema angekuwa Rais Clinton angekuwa jela, clinton aomba radhi lakini…
Waziri wa Ajira Aipongeza NEC Kwa Ubunifu