Marekani imeoionya Uturuki kuhusu mpango wake wa kutaka kuwashambulia wanamgambo wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani huku Uturuki ikiwachukulia kama magaidi.

Trump amesema kuwa kama Uturuki itathubutu kuwashambulia wanamgambo hao, itauharibu uchumi wa Uturuki, hivyo imeonya kutochukuliwa kwa hatua zozote za kijeshi dhidi ya wanamgambo hao wakati ambapo Marekani inaviondoa vikosi vyake nchini Syria.

Msemaji wa Rais wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan, Ibrahim Kalin aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba hakuna tofauti kati ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu na wanamgambo wa Kikurdi wa YPG na kwamba Uturuki itaendelea kupambana na magaidi wote hao.

Aidha, hayo yamejiri mara baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuonya hapo Jumapili kwamba atailemaza Uturuki kiuchumi iwapo itafanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao.

Hata hivyo, Uturuki inalichukulia kundi la YPG kama magaidi waliotokana na chama cha Wakurdi cha PKK ambacho kimekuwa kikifanya mashambulizi dhidi ya Uturuki tangu mwaka 1984. Chama cha PKK kimeorodheshwa na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya kama kundi la kigaidi. Lakini katika siku za hivi majuzi Marekani imekuwa ikishirikiana na YPG kwa kuwapa usaidizi wa kijeshi na mafunzo katika kupambana na kundi la Dola la Kiislamu.

Kesi ya 'Uchochezi' inayomkabili Zitto Kabwe yaota Mbawa
Kigwangalla amkubali Fatma Karume, naye anena

Comments

comments