Marekani imesema kuwa vikosi vyake vimefanya mashambulizi ya makombora ya anga kulenga kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia na kuwaua askari 24 wa kundi hilo.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa jana na Komandi ya Marekani barani Afrika, mashambulizi hayo yalifanyika katika maeneo ya Shebeeley, mkoa wa Hiran, katikati ya Somalia.

“Mashambulizi ya kijeshi ya ndege ni sehemu ya mikakati yetu. Mashambulizi haya yanawasaidia washirika wetu kupiga hatua kubwa katika kupambana na Al-Shabaab ikiwa ni pamoja na kutwaa maeneo ambayo yalikuwa yanadhibitiwa na magaidi hawa,” imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Komandi ya Marekani barani Afrika, Meja Jenerali Gregg Olson.

Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga mara kadhaa katika kuunga mkono vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyosaidia Serikali ya Somalia kupambana na A-Shabaab kwa miaka kadhaa.

Mwaka jana, Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi 45 ya anga ikiwa ni zaidi ya mashambulizi 35 yaliyofanyika mwaka jana.

Al-Shabaab wameendelea kufanya vitendo vya kigaidi nchini Somalia ikiwa ni miaka kadhaa tangu wafurushwe kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Kundi hilo linalenga kuiondoa madarakani Serikali ya kidemokrasia ya Somalia na kupandikiza utawala wa dini.

Davido jukwaa moja na Cardi B, Future
Video: Makonda aanika ya wasanii, 'hakuna asiyejua mmefulia'