Marekani imeitungua ndege ya kijeshi ya Syria iliyokuwa ikijiandaa kuwashambulia wanamgambo wa IS ambao wamekuwa wakihatarisha maisha ya wananchi wa nchi hiyo huku umoja wa mataifa ukitaka kuwepo na usuluhishi.

Aidha, Marekani imesema kuwa imefikia hatua hiyo mara baada ya jeshi la Syria kuvishambulia vikosi vya Syrian Democratic Force SDF, vinavyoungwa mkono na nchi hiyo kwa lengo la kupambana na wanamgambo wa Islamic State.

Kwa upande wa Serikali ya Syria imesema kuwa ndege yake ilikuwa katika maandalizi ya kuwashambulia wanamgambo wa Islamic State na si vikosi vya Syrian Democratic Force vinavyoungwa mkono na Marekani.

Vikosi vya Syrian Democratic Force (SDF ) vinaungwa mkono na umoja unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana na wanamgambo wa Islamic State ambao wamekuwa tishio katika ukanda huo.

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 19, 2017
Video: Nchemba amvaa Lissu makinikia ya Acacia, Hali si shwari mgodi wa North Mara