Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amekanusha taarifa inayosema kuwa Marekani inataka kurejea kwenye Meza ya mazungumzo na Korea Kaskazini.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha matangazo cha CBS kilichopo nchini Marekani, Pompeo amesema kuwa Marekani ilifahamu kuwa mazungumzo hayo yangekuwa magumu.

Aidha, alipoulizwa iwapo Marekani ina wasi wasi juu ya makombora ya masafa mafupi yanayofyatuliwa na Korea Kaskazini, Pompeo amesema ni kweli nchi hiyo ina wasi wasi na angependelea Korea Kaskazini iache mara moja kufanya hivyo.

Wakati huo huo, Pompeo amekiri kuwa Wanamgambo wa Dola ya Kiislam wanapata nguvu katika baadhi ya maeneo, lakini amesema kuwa uwezo wa Wanamgambo hao kufanya mashambulio umepungua.

Hata hivyo, Pompeo ameongeza kuwa kuna baadhi ya maeneo kundi hilo la ISIS lina nguvu kuliko miaka mitatu au minne iliyopita.

Mwanaharakati ahukumiwa kwenda jela maisha
Mkurugenzi wa ATCL afunguka kuhusu Bombardier iliyoharibika