Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema kuwa nchi hiyo haina uadui wowote na Korea Kaskazini huku akiwatoa hofu wananchi kuhusu mpango wa majaribio ya silaha za nyuklia wa Pyongyang.

Amesema kuwa Marekani haina mpango wowote kuhusu kufanya mabadiliko ya utawala wa Korea Kaskazini hivyo watu hawatakiwi kuwa hofu yoyote ya kuzuka mapigano kati ya nchi hizo.

” Hatutaki mabadiliko ya utawala wala hatuna lengo la kuuangusha utawala wa Korea Kaskazini, na wala hatuna mpango wa kuharakisha muungano wa eneo la Peninsula, na Serikali yetu haijapanga chochote kuhusu kupeleka wanajeshi kwenye eneo la Korea Kaskazin,”amesema Tillerson

Aidha, Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi Nchini Marekani Pentagon, ilitoa taarifa hivi karibuni juu ya hatua za kijeshi , lakini wakati huo huo wachambuzi wameonya hatua hivyoi kwa kusema kuwa kukabiliana na Korea Kaskazini itakuwa ni maafa.

Hata hivyo, Majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini yamesababisha hofu kubwa juu ya tishio la serikali ya Pyongyang dhidi ya Marekani , na kuzingatiwa kwa haja ya kuzuia shambulio lolote nchini Marekani.

Halmashauri Rukwa zaonywa dhidi ya matumizi mabovu ya mashine za EFD
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 2, 2017