Zaidi ya wanamgambo 100 wa Al-Shabaab, ikiwemo makamanda 20 kusini magharibi mwa Somalia wameuawa kufuatia shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na Marekani.

Wakati taarifa hizo zikiendelea kuenea, Marekani imekanusha ripoti hiyo na kueleza kuwa jeshi lake halikufanya shambulizi hilo dhidi ya wanamgambo 100 wa Al-Shabaab.

Marekani imetoa kanusho hilo kupitia kitengo chake cha Africom kinachosimamia operesheni za kupambana na ugaidi katika bara la Afrika, ambapo kimekanusha kufanya shambulizi hilo na kusema kuwa ilifanya shambulizi dhidi ya Al Shabaab nchini Somalia mara ya mwisho mwezi Januari mwaka huu.

“Marekani haijatekeleza shambulizi lolote katika eneo hilo. Shambulizi letu la mwisho lilifanywa mwezi Januari,” wamesema Africom.

Makamanda wakuu wa Al-Shabaab akiwemo Abdirahman Fillow na Abdirahman Ben Dutie waliuawa katika shambulizi hilo katika eneo la El-Adde.

Africom imesema kuwa kikosi kidogo cha wanajeshi wake wako nchini Somalia ili kutoa mafunzo kwa jeshi la taifa hilo na kuliwezesha kupambana na Al-Shabaab.

Wawili Kutangulia Nusu Fainali Ligi Ya Mabingwa Ulaya
Shauri La Kagera Sugar Halilali