Watu watatu wameuawa na wengine takribani 30 wamejeruhiwa vibaya leo katika mji wa Hesston nchini Marekani baada ya kufyatuliwa risasi na mwanaume mmoja aliyekuwa kwenye gari.

Polisi wa eneo hilo wameeleza kuwa mwanaume huyo aliyekeleza shambulio hilo baya aliuawa papo hapo na maafisa wa usalama.

Mkuu wa polisi wa  eneo hilo, T. Walton alilielezea tukio hilo kuwa ni baya kuwahi kutokea katika mji huo na wilaya ya Harvey.

“Tunaendelea kulitatua tatizo hilo.Mnapaswa kuwa makini,tunaenda kujaribu kupata taarifa zote kwa hali na mali, kuna wengi ambao watakutana na majonzi kabla ya haya yote kuisha,” alisema mkuu huyo wa Polisi.

Polisi wamemtaja mshambuliaji huyo kwa jina la Cendric Larry Ford mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Newton na alikuwa muajiriwa wa kampuni ya Excel Industries. Aliwapiga risasi watu 15 na kuwajeruhi vibaya huku wengine wakijeruhiwa wakati wa purukushani za kujiokoa.

Matukio kama haya yamekuwa yakiripotiwa mwaka jana nchini Marekani, hali iliyopelekea rais wa nchi hiyo, Barack Obama kumwaga machozi wakati akitetea muswada wa sheria ya kudhibiti umilikaji silaha inayoweka masharti magumu.

Chanzo: abc news.

FIFA Kumpata Rais Mpya Hii Leo
Wasira: Nilianza kupigwa picha tangu natoka chooni, nahisi huyu katumwa