Serikali ya Marekani imemtaja Mtanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu kwa jina la ‘Shikuba’ kuwa kinara wa dawa za kulevya duniani na imemchukulia hatua kali za kuufyeka mtandao wake pamoja na kutaifisha mali zote zilizoko nchini humo.

Serikali ya Marekani imeeleza kuwa inamtambua Shikuba kama kinara wa usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia Sheria ya Utambuzi wa Vinara wa Dawa za Kulevya wa Nje (Foreign Narcotics Kingpin Designation Act) ya Marekani).

Taarifa rasmi ya Marekani iliyotolewa juzi ikiwa na picha ya Mtanzania huyo, ilieleza kuwa ni kinara wa kimataifa wa dawa za kulevya anayesafirisha mamilioni ya tani za heroine na cocaine kwenda Afrika, Marekani Kaskazini, Asia na kwamba mtandao wake mkuu uko Afrika Mashariki.

“Kutokana na uamuzi wa leo (juzi), mali zote za Hassan na mtandao wake ambazo ziko ndani ya mamlaka ya Marekani au kwenye mikono ya raia wa Marekani zinataifishwa,” inasomeka taarifa hiyo ya Serikali ya Marekani.

Kumbukumbu za Jeshi la Polisi nchini Tanzania zinaonesha kuwa alikamatwa mwaka 2014 hapa nchini, akihusishwa na shehena ya kilo 210 za heroin zilizokamatwa mkoani Lindi mwaka 2012.

Aliyekuwa Kamishna wa Kikosi cha Kupambanana Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Mzowa ameeleza kuwa Jeshi la Polisi lilimkamata Shikuba Januari mwaka 2014 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), baada ya kumtafuta muda mrefu huku mbinu za jeshi hilo zikigonga mwamba.

Kamanda Mzowa alisema kuwa endapo itathibitika kuwa Tajiri huyo wa unga alipata mali zake kwa njia ya kuuza dawa hizo za kulevya, mali zake zote zitataifishwa kama Marekani walivyofanya.

Polisi aliyejichanganya kwa Mtuhumiwa wa Mauaji afukuzwa kazi
Rufaa ya Babu Seya na Mwanae kuanza kutiririka leo Mahakama ya Afrika