Nchi ya Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya virusi vya Corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Kwa upende wa rais Trump amesema amepokea kwa masikitiko taarifa hiyo

Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.

Lakini kuna vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani kuwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

Uganda: Polisi wamewapiga risasi waliotumia usafiri wa Umma
Ummy Mwalimu: ''Makonda amemkosea Mbowe''