Wawakilishi wa Marekani na China wamekamilisha mazungumzo yao jana bila kutoa maelezo ya matokeo ya mikutano yao.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin amesema kuwa mazungumzo yao yalikuwa mazuri, huku Naibu waziri Mkuu wa China, Liu He akisema kuwa yalimalizika vyema

Aidha inasemekana kuwa wajumbe hao wamekubaliana kuendelea na mazungumzo hayo jijini Beijing katika siku zijazo.

Mazungumzo hayo yamekuwa mazito na magumu kutokana na tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa atapandisha ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200 zinazoingizwa Marekani.

Hata hivyo, hatua hiyo ilianza kutekelezwa jana Ijumaa. baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya jana, Trump aliwataka maafisa wa biashara wa Marekani kuanza mchakato wa kupandisha ushuru kwa bidhaa zilizobaki za thamani ya dola bilioni 300 zinazoingizwa Marekani kutoka China.

 

Msaada wa dharula wahitajika Congo DRC
Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma TPSC watakiwa kuwa waadilifu

Comments

comments