Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump anashutumiwa kwa ongezeko la matendo ya kigaidi dhidi ya waislam kufuatia matukio mbalimbali wanayofanyiwa wafuasi hao wakiwa nchini Marekani.

Utafiti uliofanywa na kikundi cha Waislam Council on American-Islamic Relations (CAIR) uliotolewa Jumatatu umebainisha kuwa kumekuwa na ongezeko la 15% ya uhalifu kwa Waislam waishio Marekani unaosababishwa na chuki.

Ambapo matukio mbalimbali yametumika kupata majibu ya tafiti hiyo yakiwemo kupigwa kwa mwanamume wa Kiislam katika eneo la Bronx la mji wa New York kwa kushambuliwa na watu waliomwita gaidi, tukio jingine ni la mwezi Novemba ambapo mgahawa unaomilikiwa na familia ya Kiislam, Kansas ulichomwa moto.

Taasisi hiyo ya Kiislam CAIR imeeleza ongezeko hilo linatokana na sera za Rais wa Marekani Donald Trump, na hasa katazo la wahamiaji kutoka nchi zilizo na Waislam walio wengi.

“Hakujawahi kuwepo kitu kama hivi abadan, kwa jumuiya ya Waislam kuwa ni wanyonge wa Rais wa Marekani ambaye amekuwa akiwashambulia,” amesema Gadeir Abbas, wakili wa CAIR.

Msemaji wa White House, Kelly Love amejibu tuhuma hizo akidai kuwa Utawala wa Trump unafuata sheria na unachukia aina zote za uvunjaji sheria ikiwemo uhalifu unaotokana na chuki.

” Rais Trump ameendelea kulaani uvunjifu wa amani, ubaguzi na makundi yenye kutengeneza chuki.” amesema Kelly Love

Wakati akiwa mgombea wa urais, Trump aliahidi “kusitisha kabisa kuingia Waislam nchini Marekani.” Mara baada ya kuingia madarakani alisaini amri ya kiutendaji ikipiga marufuku wasafiri kutoka nchi kadhaa zenye Waislam walio wengi kuingia Marekani.

Amri hiyo ambayo ilifanyiwa marekebisho, na kuiingiza Korea Kaskazini, ilianza kutumika mwisho wa mwaka 2017.

Fatuma alia na uhaba wa mawakili, wakili mmoja wateja 25,000
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 24, 2018