Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu WizKid ametangazwa rasmi kuweka rekodi ya kuuza jumla ya nakala Laki tano za album yake Made in Lagos ya mwaka 2020.

Mapema Jumatatu ya Agosti 29, 2022, Recording Industry Association ya huko nchini Marekani, ilithibitisha kwa kutanzagaza kuwa albamu ya mwimbaji huyo ‘Made In Lagos’ bimefanikiwa kuuza nakala zaidi ya laki tano (500,000) kwa nchini Marekani.

Hatua hii kubwa inampa Wizkid heshima ya kipekee ya kuwa msanii pekee wa Nigeria na Afrika ambaye albamu yake imeuza zaidi ya nakala 500,000 huko nchini Marekani.

Ayodeji Ibrahim Balogun ‘WizKid’ Picha na Instagram.

Suala la rekodi hiyo mpya iliyowekwa na muimbaji huyo imewaibua mashabiki pamoja na wadau mbali mbali wa muziki wakiwamo wanahabari wamemmwagia sifa Wizkid, kwa kufanikiwa kuiweka Nigeria na Afrika kwa ujumla kwenye ramani, huku akionekana kuwa chachu ya kuongeza kasi wasanii wengine.

Ukubwa wa album hiy kwa zaidi ya asilimi sabini na tano (75%) unaadaiwa kusababishwa na wimbo maarufu ‘Essence’ aliomshirikisha Tems, wimbo ulijizolea umaarufu mkubwa kote duniani.

‘Essence’ ni moja ya nyimbo kutoka kwenye album hiyo uliofanikiwa sana kupenya na kupokelewa vizuri nchini Marekani na kuchochewa na Remix ya wimbo huo aliyoshirikishwa nyota wa Pop kutoka Marekani Justin Bieber, ambayo ilifanikiwa nafasi ya 9 kwenye chati ya Billboard Hot 100 na platnumz mara mbili.

kitendo cha kuthibitishwa kwa ‘Made In Lagos’, mashabiki wa Wizkid watakuwa na matumaini makubwa kwamba albamu nyingine zinaweza kufuata hatua za album hiyo, kwa matarajio ya kuendelea kuliteka soko kimataifa huku muziki wa Afrobeats ikiendelea kupaa zaidi kimataifa.

Billnas, Nandy rasmi sasa ni wazazi
Serikali yaainisha fursa za uwekezaji sekta ya Madini