Serikali ya Marekani imefunga baadhi ya shughuli zake baada ya Baraza la Seneti kushindwa kupitisha mswaada wa matumizi ya serikali. hivyo kupelekea kusimama kwa shughuli zisizo za lazima,

Baadhi ya Maseneta Warepublican walijiunga na sehemu kubwa ya Wademokratic kupinga mswaada huo, ambao ulihitaji kura 60 kupita katika baraza hilo lenye wajumbe 100.

Aidha, kushindwa kufikia makubaliano siku ya Ijumaa, Maseneta wa Bunge la Marekani sasa watalazimika kuwa na majadiliano ya dharura ndani na nje ya bunge kupata makubaliano ya mwisho ambayo yatapitisha matumizi ya serikali.

Hata hivyo, kwa mara ya mwisho serikali ya Marekani ilifunga shughuli zake kwa siku 16 baada ya kukosa fedha za matumizi mwaka 2013 katika utawala wa Rais Barack Obama.

Video: Vurugu kubwa zaibuka Kigamboni, Kivumbi Kinondoni na Siha
Chama cha SPD kuamua juu ya kuungana na Merkel