Nchi ya Marekani, ni moja ya nchi ya kimataifa iliyositisha msaada nchini Sudan na kuomba serikali ya kiraia irejeshwe, hali hiyo imejiri baada ya Jenerali Mkuu wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan kutangaza hali ya hatari na kuivunja serikali hatua iliyolaaniwa na jamii ya kimataifa. 

Umati wa watu umefanya maandamano hadi jana usiku nchini Sudan kupinga mapinduzi ya kijeshi, huku vurugu zikiugubika mji mkuu Khartoum baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji.

Takriban watu 10 wameripotiwa kuuawa na wengine makumi kadhaa kujeruhiwa, wengi wao ikiwa ni kutokana na risasi zilizofyatuliwa na wanajeshi kwenye makundi ya waandamanaji

Umoja wa Mataifa umetaka kuwachiwa huru mara moja kwa waziri mkuu Abdalla Hamdok. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura leo kujadili mzozo huo wa Sudan. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu pia wamelaani mapinduzi hayo

Simba SC yapelekwa Zambia
Kocha Gomes afungasha virago