Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson  ametoa wito kwa nchi ya Qatar na majirani zake kumaliza mgogoro wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda wa wiki kadhaa.

Amesema kuwa Qatar imeanza kupitia mapendekezo na masharti iliyowekewa na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu ili kuweza kutatua tofauti zilizojitokeza.

“Qatar imeanza kupitia orodha ya mapendekezo na matakwa yaliyowasilishwa na Bahrain, Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, ingawa kuna baadhi ya vipengele ni vigumu sana kuafikiwa na Qatar lakini kuna maeneo muhimu ambayo yanatoa fursa ya kuendelea kwa mazungumzo”amesema Tillerson.

Hata hivyo, Rais wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan  amekataa madai ya nchi hizo za Umoja wa Falme za Kiarabu kuitaka nchi hiyo kuondoa wanajeshi wake kutoka Qatar  ikiwa ni moja ya masharti mengine magumu iliyoyataja Marekani kutekelezwa na Qatar.

 

 

Binti wa Sassou Nguesso kitanzini kwa rushwa
Ifahamu saikolojia ya ubongo