Ndege aina ya B-1 za kivita za Marekani zenye uwezo wa kubeba makombora yenye mabomu ya nyuklia au mabomu ya nyuklia yenye uwezo wa kuharibu hata mahandaki zimepaa juu ya anga ya Korea Kusini.

Hayo ni kufuatia siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la tano la silaha za nyuklia ambapo Marekani imeitahadharisha Korea Kaskazini kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taifa hilo baada ya kufanyika kwa majaribio hayo ya bomu Ijumaa.

Jaribio hilo la Pyongyang ndilo kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na taifa hilo.

Ndege za Marekani zilipaa si mbali sana kutoka ardhini juu ya kituo cha kijeshi kinachopatikana kilomita 77 kutoka mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.

El-Hadji Diouf: Nilimwambia Balotelli Asiende Liverpool
Vadim Vasilyev Azishutumu Man Utd, Chelsea