Wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Italia Mario Balotelli (Mino Raiola), amesema anaamini ipo siku mchezaji wake atarejea kucheza soka katika ligi ya nchini England (PL).

Raiola ambaye ni wakala wa wachezaji wenye majina katika ligi za barani Ulaya akiwepo Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic ametanabaisha hayo kutokana na ubora wa kiwango cha Balotelli akiamini bado ana uwezo mkubwa wa kucheza katika klabu kubwa.

Kwa nyakati tofauti Balotelli ameshacheza kwenye ligi ya nchini England (PL) katika klabu za Manchester City na Liverpool na amepitia changamoto kadhaa.

“Ufaransa inamuhitaji kama walivyokuwa wakimhitaji Zlatan. Yupo vizuri lakini ipo siku atarejea katika ligi ya nchini England (PL).” Alisema Raiola

Balotelli alisajiliwa na klabu ya Nice baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp jambo ambalo lilipelekea kumueleza bayana hamuhitaji katika kikosi chake.

“Mario na Jurgen Klopp hawakupata nafasi kufanya kazi pamoja na Klopp hakutaka kumpa nafasi hiyo, Klopp alikuwa akimuona Balotelli kama mpuuzi tu.”Aliongeza Raiola.

Tanzania yaongoza duniani kutoa huduma za fedha kupitia simu
Claudio Ranieri Asisitiza Heshima Kwa N'Golo Kante