Meneja mpya wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, Carlo Ancelotti amekubali kumuweka sokoni kiungo mshambuliaji Mario Gotze kwa kutaja tahamani ya ada yake ya uhamisho kuwa Pauni million 35.

Chelsea walitangulia katika mpango wa kutaka kumsajili kiungo huyo aliyeipa ubingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani, kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Argentina mwaka 2014 kule nchini Brazil.

Ancelotti ambaye aliwahi kufanya kazi huko Stamford Bridge, anaamini thamani ya Pauni million 35, inawezekana kwa kiungo huyo na huenda ikawa rahisi kwa klabu ya Chelsea kumsajili na kutimiza malengo yake chini ya utawala wa meneja Antonio Conte.

The Blues wameripotiowa kutenga kiasi cha Pauni million 100, ambazo zitatumika katika mipango ya kufumua na kukisuka upya kikosi chao, ambacho kwa msimu huu hakikufanya vyema.

Antonio Conte has been offered Mario Gotze by Carlo Ancelotti Mameneja wapya wa klabu za Chelsea na FC Bayern Munich, Antonio Conte (Kushoto) na Carlo Ancelotti (Kulia).

Meneja Antonio Conte, ameshahakikishiwa uwepo wa fedha hizo, na ametakiwa kufanya kazi ya usajili ambao utamsaidia katika hatua ya kurejesha heshima huko magharibi mwa jijini London.

Hata hivyo Gotze, anatajwa kuwa katika rada za aliyewahi kuwa bosi wake wakati akiwa na klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ambaye kwa sasa anatoa huduma ya ukufunzi nchini England akiwa na klabu ya Liverpool.

Jurgen Klopp is also willing to splash out to get Mario Gotze to Liverpool Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp alipokua kwenye klabu ya Borussia Dortmund, akisaliamiana na Mario Gotze katika moja ya michezo ya ligi ya nchini Ujerumani.

Kwa mantiki hiyo inadhihirisha kwamba, thamani ya Gotze pia itawahusu majogoo wa jiji kama kweli watakua na mipango ya kumsajili.

Klopp, anaamini kama atafanikiwa kumnasa Gotze, kikosi chake kitaimarika maradufu kwa msimu ujao wa ligi ya nchini England ambao umeshatabiriwa kuwa na mshike mshike mkali.

Mesut Mustafa Ozil Kubembelezwa Kwa Mkataba Mpya
Silvio Berlusconi Kukutana Na Wafanyabiashara Wa China

Comments

comments