Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limemtangaza mwamuzi kutoka nchini England, Mark Clattenburg kuwa msimamizi mkuu wa dakika 90 za mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani humo, ambao utashuhudia Real Madrid wakipapatuana na Atletico Madrid Mei 28 mjini Milan nchini Italia.

Clattenburg mwenye umri wa miaka 41, ametangazwa na kupewa jukumu hilo, kutokana na hatua ya kuonyesha kiwango kizuri cha uchezeshaji kwa msimu huu, na inaaminiwa atatoa haki katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wote wa soka duniani.

UEFA pia wamemtangaza mwamuzi kutoka nchini Sweden, Jonas Erksson mwenye umri wa miaka 42, kupuliza filimbi katika mchezo wa hatua ya fainal ya Europa League.

Mchezo huo utashuhudiwa majogoo wa jiji Liverpool wakipambana na mabingwa watetezi Sevilla CF kutoka nchini Hispania, Mei 18 katika uwanja wa St Jacob Park uliopo mjini Basel nchini Uswiz.

Joe Ledley Kuzikosa Fainali Za Ulaya (Euro 2016)
Rais Magufuli atua kwa Museveni

Comments

comments