Mwamuzi aliyejizolea umaarufu mkubwa barani Ulaya Mark Clattenburg ametangazwa kuwa msimamizi wa sheria 17 za mchezo wa mahasimu wa mjini Manchester, Man Utd dhidi ya Man City uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Old Trafford.

Pep Guardiola na Mourinho wanakutana kwa mara ya kwanza wakiwa katika klabu zenye uhasimu mkubwa bila kusahau uhasama walio nao tangu wakiwa katika ligi ya nchini Hispania (La Liga).

Ikumbukwe wawili hao hawajapoteza wala kutoa sare hata mchezo mmoja, ikiwa wameanza ligi kwa ushindi wa asilimia 100.

Manchester City watamkosa mshambuliaji wao tegemezi Sergio Aguero baada ya kufungiwa michezo mitatu kufuatia kumpiga kiwiko beki wa kati wa West Ham Winston Reid.

Mike Dean ametajwa kama kamishna wa wa mchezo (fourth official), wakati Jake Collins na Steve Bennett watakuwa pembeni kushika vibendera.

Clattenburg alichezesha fainali ya UEFA Champions League  2015-16 na Euro 2016 na kupewa tena mchezo huu ambao unahesabika kama mchezo wenye ushawishi wa aina yake kwenye ligi ya EPL.

Video: Majibu ya Serikali kuhusu upungufu wa vifaa tiba na wataalamu hospitali za Jeshi
Video: Kamanda Sirro akionyesha silaha za kivita zilizokamatwa