Mwamuzi Mark Clattenburg ataendelea kuchezesha michezo ya ligi kuu ya soka nchini England hadi mwishoni mwa msimu huu.

Juma lililopita mwamuzi huyo alitangaza kuachana na ligi hiyo baada ya kupata ajira mpya Saudi Arabia ambapo atakua mkuu wa jopo la waamuzi nchini humo.

Bodi ya ligi nchini England imemteua Clattenburg kuchezesha mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili kati ya  West Brom dhidi ya AFC Bournemouth utakaochezwa The Hawthorns.

Pia imefahamika kuwa, mwamuzi huyo ataendelea kuteuliwa kuchezesha michezo mingine ya ligi hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu, ambapo atakua huru kuelekea katika majukumu yake mapya nchini Saudi Arabia.

Clattenburg mwenye umri wa miaka 41, anakwenda Saudi Arabia kuchukua nafasi ya mwamuzi mwenzake kutoka England Howard Webb, ambaye ameamua kustaafu na kurejea nyumbani.

Clattenburg ataendelea kukumbukwa kwa kazi nzuri aliyoifanya msimu uliopita, ambapo alichezesha kwa ufasaha michezo ya hatua ya fainali ya michuano ya kombe la FA, ligi ya mabingwa barani Ulaya na Euro 2016.

Christian Bassogog Atimkia China
Maalim Seif amtaka Shein kujing'oa madarakani