Kiungo na nahodha wa West Ham Utd, Mark Noble amethibitisha kuwa na uhusiano mbaya na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Dimitri Payet kwa kipindi cha majuma matatu sasa.

Noble amethibitisha taarifa hizo kufutia mgomo uliowekwa na Payet wa kukataa kufanya mazoezi sambamba na kucheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Crystal Palace ambapo West Ham Utd walichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Noble mwenye umri wa miaka 29 amesema,“nimekua hapa katibu maisha yangu yote ya soka na sijawahi kukutana na kitu kama alichokionyesha Payet, jambo hili limenisikitisha sana na nikwambie tu hatuzungumzi kwa majuma matatu sasa.

“Sizungumzi nae kwa sababu naona hakuna haja ya kufanya hivyo, kutokana na jambo hilo kunikera na wakati mwingine halina misingi ya kushinikiza kutaka kuondoka,” alisema.

“Tupo hapa kwa lengo la kuisaidia timu ili ifanye vizuri, sasa kila mmoja anapoanza kuleta mambo yake binafsi tena kwa kuamini bila yeye hatuwezi kufanya jambo inaumiza sana,” aliongeza.

Hata hivyo, Noble amemtaka meneja wake, Slaven Bilic kuwa mstahamilivu kwa kuhakikisha analimaliza jambo hilo kwa kutumia busara na hekima ili kila mmoja atambue umuhimu wake anapokua katika kikosi kama cha West Ham Utd.

Payet anaamini kipindi hiki ni kizuri kwake kuondoka katika kikosi cha West hama Utd kufuatia kiwango chake kushawishi baadhi ya viongozi wa klabu kubwa barani Ulaya.

Payet alionyesha uwezo mkubwa msimu uliopita akiwa na West Ham utd, na hata alipoitwa kwenye kikosi cha Ufaransa wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016) alionyesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kufika hatua ya fainali.

Majaliwa azindua safari za ATCL Dar/Dodoma, atoa wito
Stereo amuomba penzi Chemical kwa magoti