Klabu ya Middlesbrough ipo tayari kuwasilisha ofa ya usajili wa beki kutoka nchini Slovakia na klabu ya Liverpool, Martin Skrtel.

Klabu ya Middlesbrough ambayo itashiriki ligi kuu ya England msimu ujao, inajiandaa kutuma ofa ya Pauni milioni 6, huko Anfield yalipo makao makuu ya Liverpool.

Meneja wa Middlesbrough Aitor Karanka, amedhamiria kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 31, kutokana na kuridhishwa na kiwango chake ambacho anaamini kitaisaidia The Boro.

Hata hivyo huenda Aitor Karanka, akapata upinzani mkali, kutoka kwenye klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki ambayo imeonyesha nia ya kumsajili Skrte.

Wakala wa Skrtel, Karol Csonto amesema mpaka sasa klabu hizo mbili zimeonyesha nia ya dhati kutaka kumsajili mchezaji wake, lakini maamuzi ya mwisho yatatolewa siku za karibuni.

Skrtel, amesaliwa na mkataba wa miaka miwili na amekuwa katika hatua ya kuhitaji changamoto mpya ya kucheza soka lake, hasa baada ya kuonekana kuna ugumu wa kwenda sambamba na mfumo wa meneja mpya wa Liverpool, Jürgen Klopp.

Jurgen Klopp Kumfungulia Milango Pepe Reina
Angalia Orodha Ya Wachezaji 552 Watakaocheza Fainali Za Euro 2016