Waziri wa Usafirishaji wa Kenya, Kipchumba Murkomen amesema safari za anga za shirika la ndege la Kenya (Kenya Airways), hii leo (Novemba 5, 2022), zimevurugika kutokana na mgomo wa marubani wakishinikiza mazingira mazuri ya kazi.

Hatua hiyo, imesababisha ndege kadhaa kushindwa kufanya safari zake, hali ambayo imewaathiri maelfu ya abiria na Waziri huyo mpya wa usafrishaji amewaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege kuwa mgomo huo haukuwa na msingi.

Baadhi ya abiria mbao wamekutana na adha ya usafiri wa anga kutokana na mgomo wa Marubani. Picha ya BBC.

Shirika la ndege la Kenya, ambalo linamilikiwa kwa sehemu fulani na serikali ya Kenya pamoja na lile la Ufaransa, Air France na la Uholanzi, KLM, ni mojawapo ya mashrika makubwa zaidi ya usafiri wa anga barani Afrika, linaloziunganisha nchi nyingi za Ulaya na Asia, lakini linakabiliwa na misukosuko, ikiwa ni pamoja na kukabiliwa na hasara kwa miaka kadhaa.

Jana, Novemba 4, 2022 Marubani wa shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, walitangaza kuanza mgomo hii leo Jumamosi (Novemba 5, 2022), kutilia mkazo madai yao ya mazingira bora ya kazi, licha ya mahakama ya nchi hiyo kuamuru mgomo huo usitishwe.

Zelensky ajipa matumaini vita yake na Urusi
Moto waporomosha paa la klabu, 13 wafariki