Serikali nchini Kenya, inatarajia kutumia zaidi ya dola 156 milioni kununua vifaa vya kupambana na ugaidi na uhalifu mwingine huku ikipiga marufuku wafugaji kuchunga mifugo na silaha.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Taifa hilo, William Ruto ambaye amesema marufuku hiyo itaendana na zoezi la kukusanya silaha zote wanazomiliki wafugaji isivyo halali kwa lengo la kupunguza matukio ya uhalifu.

Rais wa Kenya, William Ruto.

Amesema, “kuanzia sasa, hakuna mtu atakayeruhusiwa kuchunga akiwa na silaha. Silaha ni za maafisa wa usalama tu na msamaha wa kusalimisha bunduki kwa hiari ulikwisha tarehe 21 Februari na 19 pekee.”

Katika kufanikisha zoezi hilo, tayari Wanajeshi na Polisi nchini humo wanaendesha operesheni katika kaunti 10 za maeneo ya kaskazini, ambapo wizi wa ng’ombe umekuwa ukichochea kuenea kwa silaha haramu na kufanya uwepo wa ukosefu wa usalama kwa miaka mingi.

Uchaguzi Nigeria: Wapinzani wasusa kuhesabu kura
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 28, 2023