Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi amesema kuwa hata sita kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki binasfi wa magari watakao kufunga vingora kwenye magari yao kinyume na sheria

Kamanda Ng’anzi ameyasema hayo wakati akizindua wiki ya usalama barabarani.

”Sheria ya usalama barabarani inatambua baadhi ya magari ambayo yanatakiwa yawe na ving’ora na vimulimuli na hayahusiki katika mwendo wa dharura kuanzia leo tutawakamata na tutawashitaki kwa kuweka vitu ambavyo haviruhusiwi”

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wakati wa zoezi la ukaguzi wa magari linaloenda na wiki ya usalama ya usalama Barabarani yenye kauli mbiu isemayo mkinge mwenzako na ujikinge mwenyewe ili kujiepusha na ajali za barabarani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Fredinand Chacha amesema watahakikisha vyombo vyote vya moto mkoa wa Mwanza vinakaguliwa.

”Nia yetu ni kwamba tuweze kupunguza ajali za barabarani kwahiyo mimi ombi langu kwa jamii ya Mwanza wote wenye vyombo vya moto tusichukue njia ya mkato ya kuchukua stika bila kukaguliwa”

Siku 11 Rubani haonekani pamoja na ndege yake.
Ugumu wa ajira ulisababisha niichukie Elimu