Mwanamuziki nguli wa Marekani anaekabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana chini ya umri wa miaka 18 Rkelly jana aliripoti mahakamani kwa ajili ya kutolea ushahidi video za ngono ambazo ziliwasilishwa na wanasheria kutoka kwenye mikono ya wasamaria wema.

Kellz akiendelea kupambana na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono taarifa mpya zinazoendelea huenda mwanamziki huyo akafunguliwa mashtaka mengine makubwa zaidi hivi karibuni.

Kwa mijibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa waendesha mashtaka wa mji wa Illinois watakaa kuanzia mwezi ujao kuzungumza na mashaidi wanaodai nguli huyo wa muziki aliwahi kufanya kosa la kuwasafirisha wasichana wadogo na kuwatumia kingono, huku wakizipitia tiketi za ndege pamoja na vyumba vya hoteli alizokuwa akiwafikishia.

Aidha wamesema kuwa  watazikusanya email pamoja na jumbe za kawaida ambazo zinaonesha namna alivyokuwa akiweka mitego ya kuwanasa ili kuwasafirisha huku uchunguzi wa phisical pia utatumika ikiwemo kuzifanyia uchunguzi nguo kama zinz sampuli yoyote ya uume wa staa huyo.

Video: Steve Nyerere - Hakuna Kaole bila ITV/Hata kama haikuwalipa, Wamuage Dk. Mengi
UN yazindua njia mpya ya kuthibiti ugaidi

Comments

comments