Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi  amemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis ameiomba mahakama kuwaachia huru chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA) na kudai DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

“Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa”, amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.

Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya (51).

Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.

Na wengine kama Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

Mwapachu aamua kustaafu Acacia
Kesi ya Masogange yapigwa kalenda