Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasilino ya Klabu ya Ruvu Shooting Masa Bwire, ameipongeza Simba SC kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa BArani Afrika, Al Ahly.

Masau ametoa pongezi hizo kwa Simba SC kupitia ukurasa wake wa Instagram, huku akiweka video ya bao lililowapa ushindi wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lililofungwana mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Luis Jose Muquissone katika kipindi cha kwanza.

Masau ameandika: “Hongereni sana Msimbazi, mumeonesha mpira wa kiwango cha hadhi ya Dunia! Mwito wangu, hizi ni mbio ndefu, MSIJISAHAU!”

“Ombi langu, Watanzania wote tuendelee kuiombea timu hii kwa Mungu, ifanye vizuri zaidi na isonge mbele katika mashindano haya makubwa Afrika.  Tusiwasahau pia Namungo FC.”

“Eeee, Mwenyezi Mungu,  twakuomba utusikie!”

Masau amekua sehemu ya wadau wa soka nchini ambao hutoa pongezi kwenye mafanikio yoyote yenye maendeleo ya soka la Tanzania, na pia hukemea pale panapojitokeza jambo ambalo sio sehemu ya ustawi wa mchezo huo.

Magufuli apanga kulivunja jiji la Dar es Salaam
TPLB yarusha kijembe Misri