Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameichimba mkwara Young Africans, kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ruvu Shooting watakua wenyeji kwenye mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Masau amese kikosi chao kimejiandaa kisawasawa kuikabili Young Africans, huku benchi la ufundi likiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza kwenye michezo kadhaa iliopita.

Amesema kutokana na maboresho ya kiufundi yaliofanywa na Kocha wao Charles Boniface Mkwassa, mashabiki wa soka hawapaswi kuwabeza kwa kutumia kigezo cha kupoteza michezo kadhaa.

“Kumekuwepo na upepo mchafu hapa katikati uliopita ambao hata sisi hatujui umekujaje na umetokea wapi, ambao kwa kiasi flani ulipunguza ile kasi yetu na matarajio yetu, ambapo baadhi ya watu walifikiria ule ndio uwezo wetu umeishia pale”

“Lakini kupitia mchezo wa kesho dhidi ya Young Africans tunahitaji watu waendelee kutuamini na kujua hii ndio Ruvu Shooting halisi na ndio maana ikaitwa Barcelona ya bongo”

“Mimi naomba niwaambie Yaoung Africans waje na tahadhari hasa mashabiki wale wanaokuja na matokeo yao kuwa iwe isiwe lazima wachukue pointi 3 kwa Ruvu Shooting, mimi niwaambie ni Jambo ambalo halitawezekana na wasije wakaisumbua red cross mara mtu amepeleka macho juu, mara mtu ameanguka na kupoteza fahamu sababu tu ya kile walichokitarajia hakikuwa ivo”

“Mimi naomba waje wakijua chochote kile kinaweza kutokea na siyo mtu anakuja na matokeo yake mkononi sijui mwingine anakuja na matokeo kichwani”

“Tunao uwezo mkubwa sana sasa hivi katika kucheza mpira, na kesho PTK inaenda kurudisha makali yake, tunaenda kuwahudumia yanga PTK kwa maana ya Papasa Tingisha Kunguta, ili Yanga waende kumaliza ligi wakiwa wanafahamu kuna kitu kinaitwa PTK na hao PTK hawakuwa na utani hivyo tunaenda kuyashuhudia kesho.

Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa. Ruvu Shooting walikubali kulala kwa mabao 2-1.

Mwenge wa Uhuru kukagua miradi yenye thamani ya bilioni 581
Shoti ya umeme yakatisha maisha ya wanandoa waliotoka fungate