Baada ya kuambulia kisago cha mabao mawili kwa moja dhidi ya vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Azam FC jana usiku, mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameibuka na kutoa taarifa za kujifariji.

Masau Bwire ambaye jana alikua jukwaani sambamba na afisa habari wa Azam FC Jaffar Iddy Maganga, ametoa taarifa hiyo baada ya kusikika akitamba kabla ya mpambano huo kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Msemaji huyo wa Ruvu Shooting ametoa taarifa hiyo na kuisambaza katika mitandao ya kijamii, ili kudhuhirisha kikosi chao kilikua na nafasi ya kuibuka na ushindi mbele ya Azam FC, na kilichowakuta ni bahati mbaya.

Hii ndio taarifa iliyotolewa na Masau Bwire.

Matokeo dhidi ya Azam bao 2-1, kwa waliofuatilia mpira, hatukupaswa, yaani yao yalikuwa yetu.

Bado natafakari, kuna nini njiani, maana, kila tukisafiri, tukiwa wenye nguvu na afya, tukiifurahia safari, tukitegemea kufika mwisho wa safari kwa kicheko,  ghafla njia inatupoteza njia…

Tupo katika kuchunguza na kutafuta ufumbuzi, huyo mdudu, mpoteza njia, tunamkanyagaje, wapi, ili tumkwepe, tusafiri salama kwa usafiri wetu wa Papasa Squared, tukiketi kwa raha zetu kwenye kiti kilichonakishiwa na Noto.

Tunaichukua hii kama moja ya pigo na jaribu. Ili uwe imara na ufikie mafanikio ya kweli, lazima ujaribiwe, upigwe mapigo ya kutosha, yanayoweza kukukatisha tamaa wewe na watu wako.

Mtumishi wa Mungu Ayubu, alijaribiwa na kupigwa kwa mapigo mengi, magumu na mazito, alisimama imara, mwisho wa siku aliyashinda.

Ruvu Shooting kama Ayubu, mtu wa Mungu, atutakatishwa tamaa, tutasimama imara, tutapambana, tutashinda.

Kumbuka, hata dhahabu, ili ing’ae, inapitishwa motoni.

Matokeo ya mchezo wa jana yameendelea kuiweka kileleni Azam FC kwa kufikisha alama 33 huku Ruvu Shooting wakishika nafasi ya 12 wakiwa na alama 16.

Msimamo kamili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2018/19 baada ya mtokeo ya michezo ya jana.

Video: Lissu atoa msimamo mzito, Mafao ya pensheni wabunge washangaa
Wakazi wa kanda ya ziwa watakiwa kuchangamkia fursa