Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Ruvu Shooting Masau Bwire amemtakia kila la kheri Haji Manara baada ya kuthibitika hatokua sehemu ya uongozi wa klabu ya Simba, kufuatia taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo Jumatano (Julai 28).

Masau amewasilisha salamu za kumtakia Kheri Manara katika Ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika: Kila la kheri, maisha ni popote, kikubwa ni weledi na nidhamu.

Kwa upande wake Haji Manara naye ameandika ujumbe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii baada ya taarifa ya kukoma kwa ajira yake ndani ya Simba SC kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Manara ameandika: Kila tunapomaliza Mechi yoyote neno langu la kwanza baada ya matokeo yoyote yale ni Alhamdulillah.

Kwa wanaofuatilia page hii wanatambua hilo.

Kwangu neno hili ndio Msamiati nnauotumia mara nyingi zaidi na hufanya hv kwa kila jambo ,liwe jema au baya.

Yes neno langu ni moja tu
AL-HAMDULILLAH

Biashara United Mara kujitosa Msimbazi
Kauli ya Hayati Magufuli inapotoshwa - Dkt. Gwajima