Afisa habari wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amejitokeza hadharani na kuchukua jukumu la kumuombea msamaha Mau Bofu, ambaye alimsababishia maumivu makali mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi katika mchezo wa mzunguuko wa 16 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara mwishoni mwa juma lililopita.

Masau Bwire amejitwisha jukumu hilo ba kuada ya kuona na kusikia kauli tofauti kutoka kwa wadau wa soka nchini, ambao wamehoji kwa nini mchezaji Mau Bofu ameshindwa kuomba radhi kwa kitendo cha kinyama alichomfanyia mshambuliaji Okwi.

Bwire ambaye ni afisa habari mkongwe, amesema mchezo wa soka ni mchezo wa kugusana, na inapotokea mmoja amemgusa mwenzie mpaka amepitiliza au amezidi kiwango kinachotakiwa, ni jambo la kawaida kuona adhabu ikitolewa kwa mhusika.

Afisa huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu wa shule ya msingi, amesema Bofu hakuwa na nia ya kumuumiza Okwi, na ndiyo maana ametambua kosa lake, hivyo anamuombea msamaha kwa Wanasimba, wadau wa soka na kwa Okwi mwenyewe ambaye ndiye aliyejeruhiwa.

“Linapotekea jambo kama hilo ni kweli muhusika anapaswa kuomba radhi, lakini kutokana na hali halisi ya tukio lilivyokua, Bofu anaendelea kujutia na ninaamini ipo siku ataomba radhi, lakini kwa sasa ninaomba nichukue jukumu la kitanguliza kauli ya kuomba msamaha kwa ajili yake”. Amesema Bwire

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu, Bofu alimpiga kwa makusudi Okwi sehemu ya shingo na kusababisha mchezaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo huku Bofu akitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Simba ilishinda mabao 3-0 katika kipute hicho kilichopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

JKT Tanzania, KMC na African Lyon zapongezwa
Vee Money ataja mamilioni yaliyotumika kutengeneza MoneyMonday