NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni Yusuph amesema kuwa wao kama Serikali hawawezi kuwaacha wananchi wakaishi kwa hofu Mkoa wa Pwani katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linafanya kazi kubwa na ya uhakika ili kurejesha hali ya amani katika maeneo hayo yaliyokumbwa na mauaji.

Aidha, ameongeza kuwa eneo hilo limepewa hadhi ya kuwa Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji ili kuweza kudhibiti hali inayoendelea kwa sasa katika maeneo hayo.

“Sisi kama Serikali tumepanga utaratibu maalumu wa kupata taarifa ili kuweza kumaliza matatizo haya ya Kibiti ili raia waendelee kuishi kwa amani kama wanavyoishi raia wengine popote nchini,”amesema Masauni.

Hata hivyo, ameongeza kuwa maendeleo ya operesheni yanayofanyika katika maeneo hayo kwa kushikilikiana na vyombo vingine vya usalama ili kuweza kuhakikisha amani inarejea katika wilaya hizo.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 1, 2017
Video: Watuhumiwa 16 mauaji Kibiti wabainika, wasakwa kila kona