Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani  Mhandisi Hamadi Masauni, amelitaka Jeshi la zimamoto na  Uhamiaji kutoshona sare zao  uraiani badala yake washone katika Jeshi  la Magereza ili kubana matumizi ya Serikali.
 Ameyasema hayo  Leo katika  ziara yake kutembelea Gereza la Ukonga ambapo amekagua  Kiwanda  cha Magereza  kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na askari Magereza.
Aidha, Masauni amewapongeza askari wa Jeshi la  Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri Serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Magereza  Kamishna Msaidizi, Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi  kama mashine za  kushonea nguo na za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendeshea shughuli za kilimo  hivyo amesema pindi Serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.

Nigeria yaanza kugawa fedha kwa raia maskini
Yemi Alade aalikwa tuzo za Grammy