Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni ametoa ufafanuzi kuhusu hoja iliyoibuliwa na Sofia Mwakagenda alipohoji juu ya tabia ya Askari Polisi inayoendelea nchini ya kukamata mtuhumiwa, kumpiga na kumtesa kabla ya kumfikisha kituo cha polisi.

Masauni amejibu hoja hiyo kwa kuikanusha na kudai kuwa kwa mujibu wa makosa ya jinai sura 20 kifungu cha 11 kimeeleza namna ya ukamataji na kwamba kifungu hicho hakiruhusu askari kumpiga na kumtesa raia wakati wowote anapokuwa kuzuizini.

Aidha ameongezea kuwa kwa kufuata kanuni za utendaji wa Jeshi la polisi askari yeyote anapobainika kufanya vitendo vya kupiga au kumtesa raia huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.

Kupitia muongozo huo, Msauni ametaja idadi ya askari ambao tayari wamekwisha adhibishwa kwa kukiuka kanuni hiyo.

”katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2017 jumla ya askari polisi 105 waliotenda makosa mbalimbali wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa pamoja na kufukuzwa kazi”. Amesema Msauni.

Mwigulu apinga kurundika vyuma chakavu
Video: Mwalimu amtakia Mtulia ‘kila la kheri’